Monday, June 30, 2014

USALAMA



Huenda usalama katika kaunti ya Mombasa ukaimarika baada ya serikali ya kaunti hiyo ,kutoa zabuni ya kununua mashini za kubaini vilipuzi ,mashine zinazojulikana kwa lugha ya kimombo “explosive trace and vapour detector”….

Katibu wa biashara kaunti ya Mombasa Mohammed Abdi amebaini kuwa mashini hizo zitakuwa na uwezo wa kujua iwapo kuna vilipuzi ama hata mabaki ya vilipuzi, na zitaweza kutumika katika maeneo yenye watu wengi ikiwemo eneo la Fery,soko la Kongowea na hata afisi zenye watu wengi.

Abdi amesema kuwa mashini hizo huenda  zikapunguza masuala ya ukosefu wa usalama katika kaunti hiyo.
Hatua hii imepokelewa vyema na wafanyi biashara katika soko hilo wakisema kuwa huenda visa vya ukosefu wa usalama  ambayvo vimekuwa vikishuhudiwa ndani ya soko hilo vikapungua.

Kauli hizi zinajiri baada ya kushuhudiwa ukosefu wa usalama ndani ya kaunti ya Mombasa,ikiwa kisa cha hivi punde zaidi ni kupigwa risasi  kwa afisa mmoja wa kitengo cha upelelezi katika eneo la Bakarani na kufariki.

No comments:

Post a Comment