Viongozi wa dini na wahubiri wa makanisa
mbalimbali katika gatuzi dogo la Likoni kaunti ya Mombasa, wamesisitiza
umoja miongoni mwa wakazi wa eneo hilo
mbali na pia kuonyesha ushirikiano na idara ya usalama ili kukabilina na visa
vya kihalifu ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika siku chache zilizopita.
Wakizungumza na waandishi wa habari
katika kanisa la Jcc huko Likoni,Joseph Maisha wa kanisa la Redeemed
amesisitiza umuhimu wa kushi kwa amani na huku akiwataka wakazi wa eneo hilo
wasigawanywe kwa misingi ya kikabila na dini.Maisha ameongeza kuwa huenda ikawa
ni ajenda za watu ambao wana malengo ya kuwagawanya wakazi hao ambao wameishi
hasa baada ya pia kushuhudiwa na vikaratasi ambavyo vimekuwa vikiangushwa na
kutia hamasa miongini mwa jamii fulani.
Wakati huo mhubiri wa dini ya
kiisilamu ambaye pia ni mshirikishi katika baraza la kiisilamu na ushauri
nchini KEMNAC Maalimu Sineno kutoka aneo la Mtongwe amesema kuwa kwa muda watu
wamekuwa wakishi kama ndugu na ina sikitisha kuona kuwa mambo kama hayo yanashuhudiwa
katika eneo hilo ila pia akahidi kuwa viongozi wa dini wanafnya kila la msingi
kushauri waumini na vijana kutojihusisha na visa kama hivyo.
No comments:
Post a Comment