GAVANA WA MOMBASA HASSAN JOHO
Baadhi ya wawakilishi wa bunge la kaunti ya
Mombasa kutoka mrengo wa ODM wamefanya mkutano mapema hii leo wakuchagua
mwakilishi wa walio wengi bungeni.hii ni baada ya wawakilishi hao kupitisha
kura ya kutokua na imani kwa aliyekua kiongozi wao Khamis mwabashiri.
Abdallah Kasagamba kutoka likoni
alichaguliwa kuwa kiongozi wa wengi katika bunge hilo.Duru za kuaminika kutoka
kikosi cha gavana wa Mombasa Hassan joho zinasema kuwa uchaguzi wa kasagamba ni
kutayarisha vijana kisiasa ili waweze kuchukua nafasi ya mbunge Masud mwahima ambaye amekuwa kiongozi kwa mda
mrefu sasa.
Duru hizo zimeongeza kuwa uchaguzi wa
Afya Rama kama mwenyekiti wakikundi cha maendeleo ya wanawake ni katika hali ya
kumtayarisha kuwania kiti cha ubenge cha mvita nafasi ambayo imeshikiliwa na
Abdulswamad Nassir kutoka ODM ambaye pia amejitoa kwenye kikosi cha joho.Rashid
Benzimba wa chama cha ODM ambaye alikua rafiki wa karibu wa joho naye pia
amejitoa kwenye kikosi hicho.
Kutokana na baadhi ya viongozi kutoka
kaunti ya Mombasa tuliyofanikiwa kuongea nao wamesema kuwa sababu kuu ya
wawakilishi hao kumuondoa mwabashiri ni kutofaulu kupitisha miswada ya chama
chao bungeni.
No comments:
Post a Comment