Huku mwezi mtukufu wa ramadhan ukiwa
katika kumi lake la mwisho, wafanyibiashara katika soko la Marikiti ndipo
wanapozidi kunogewa na biashara .
Wafanyi biashara hao wamesema kuwa
mwezi huu huwa muhimu kwao kwani biashara huimarika ijapokuwa Suala la ukosefu
wa usalama limeonekana kutia hofu watu wengi ,kutokana na mashambulizi ambayo
yamekuwa yakishuhudiwa eneo la pwani.
Aidha wamebaini kuwa wengi wa waumini wa dini
ya kiislamu wako mbioni kununulia jamaa zao mavazi, lakini wamesisitiza kuwa ni
sharti usalama uimarishwe kwani idadi ya wale wanaozuru maduka hayo wakati wa
usiku imepungua ,ikilinganishwa na msimu sawia na huu mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment