Saturday, July 26, 2014

WAITIKI



 Serikali bado inafanya mazungumzo na Waitiki anaye daiwa kuwa mmliki wa ardhi ya zaidi ya ekari mia tisa katika eneo kubwa la likoni lifaamikalo kama magwagwani. Haya yalijiri baada ya waitiki kupeleka kibali cha kumiliki adhi hiyo mara ya pili mahakamani.

Kamishna  wa polisi  kaunti ya Mombasa Nelson Marwa  alipokuwa akiwahutubia wananchi waliokuwa wamejawa na ghadhabu baada ya mahakama kutoa amri ya kuwataka  kaaji waeneo hilo kuhama. Marwa amesema kuwa mtu yeyote anayeishi katika sehemu hiyo kutokuwa na hofu.

Vilevile  mbunge wa Likoni Masoud Mwahima aliunga mkono kauli ya Marwa na kusistiza  akadai waitiki kutohangaisha wakaaji bali kushirikiana na serikali kupata suluhisho . Inadaiwa kuwa zaidi ya wananchi laki mbili na nusu wanaishi katika ardhi ya Waitiki huku zaidi ya nyumba laki moja na nusu zikiwa zimejengwa.

No comments:

Post a Comment