Serikali ya kaunti ya Mombasa ina mipango kabambe ya kuanzisha vituo vya
abiria kuabiri magari katikati ya mji na vitongoji vyake kama njia moja ya
kupunguza msongamano wa magari hiyo.
Haya ni kulingana na mwakilishi wa
wadi ya Changamwe Jimmy Odari,ambaye ameeleza kuwa ili kupunguza na kumaliza
kabisa msongamano wa magari unaoshuhudiwa kila mara katika barabara za kaunti
ni lazima kuweko na vituo maalum vya kupandia magari.
Mwakilishi huyo amesema kuwa vituo
hivyo vitahusisha matatu,piki piki na tuk tuk.
Aidha amedokeza kuwa hiyo ndio njia
pekee itakayosaidia kaunti ya Mombasa kuwa na usafiri wa haraka,akisema kuwa
upakiaji na kushukisha abiria kiholela kumechangia pakubwa kwa msangamano wa
magari.
Huenda hatua hii ya kutengea matatu
vituo vya kubeba abiria ikaleta afueni kwa madereva wa matatu kwani mara nyingi
wamekuwa wakilalama kuwa wanasumbuliwa na maafisa wa traffiki kwa kuegesha gari
mahali ambapo hapastahili.
No comments:
Post a Comment